MAENDELEO YA VIJANA
Idara ya maendeleo ya Vijana ina jukumu la kuratibu na kusimamia shughuli za maendeleo ya Vijana nchini ili kuimarisha ustawi na maendeleo ya vijana kiuchumi na kijamii.
- Kuratibu na kusimamia program za maendeleo ya Vijana Wilaya Mjini
- Kuhamasisha na kuanzisha vikundi vya kiuchumi vya Vijana
- Kufuatilia na kutoa msaada wa kitaalamu kwa vikundi vya Vijana
- Kusaidia uratibu wa Mwenge wa Uhuru katika Wilaya
- Kuwaunganisha na kuwashirikisha Vijana na fursa mbali mbali za maendeleo ya Vijana
- Kuandaa mipango na kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa program za maendeleo ya vijana katika Wilaya