Kulingana na sensa ya kitaifa ya kilimo na mifugo 2007/2008 wilaya ya Mjini haizingatiwi kama eneo la mifugo na kilimo. Walakini wachache wa wakaazi wa wilaya ya Mjini katika maeneo mengine wanajishughulisha na upandaji wa mboga (shamba la bustani). Maeneo mashuhuri ya upandaji wa mboga ni Migombani Jeshini, Kaburi kikombe, Chumbuni, Lumumba, Nyerere na Bomani.