Mkuu wa Wilaya Mjini akizungumza na Masheha wa Mjini juu ya kuwarejesha watoto walotoroka mashuleni. Mh Rashid Simai Msaraka amewataka Masheha wa Shehia zote za Wilaya Mjini walichukulie kwa uzito na kulifanyia kazi, ili kuhakikisha watoto wote waliotoroka wanarudi katika skuli zao, ili kuendelea na masomo.
Pia Mheshiwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini amempongeza Waziri wa Elimu kwa kulisimamia zoezi hilo kwa bidii yote ili kuhakikisha watoto wote wanapata haki yao ya elimu, vilevile kwa kuwapa hamasa zaidi Masheha ameitaka Wizara elimu Sheha atakae fanya vizuri zaidi katika zoezi hilo apatiwe zawadi ya pikipiki.