Ziara ya Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kukagua jengo lililoungua la Chuo cha Sayansi ya bahari Zanzibar, ziara hio Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe. Rashid Simai Msaraka amemuomba Mhe. Jakaya M. Kikwete, kuwa litakapo fanyika ukarabati jengo hilo ni lazima kuangalia masharti ya Mji Mkongwe, pia amemuomba kujengwe eneo la kuhifadhia samaki wakubwa kama vile papa, chewa na wengine na ameahidi eneo hilo litatafutwa lililo kubwa na kutosha kwa ajili ya kuvutia Utalii na uchumi wa buluu.