Wilaya ya Mjini Unguja
Mpango mkakati wa kuimarisha ufaulu wa masomo  yote katika skuli za wilaya ya mjini unguja imejipanga kukutanisha Paneli za masomo mbali mbali kuzijadili changamoto na namna bora ya kuzitatua changamoto hizo ili kuweza kurudisha hadhi ya ufaulu wa masomo.
Hayo yameelezwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mjini Mwalimu Juma Abdalla Hamad akizungumza na Walimu wa somo la Kiswahili wa Wilaya ya Mjini wanaosomesha Sekondari wa form III na form IV katika Skuli ya Sebleni, kwa lengo la kuondoa F katika somo hilo kwenye mitihani ya Taifa ya Form IV kwani wakifanya bidii inawezekana wanafunzi kupasi vizuri katika somo hilo.
Pia amewaahidi Walimu wa somo la Kiswahili wa Skuli za Sekondari za Wilaya ya Mjini kuwapatia shilingi laki moja kila mwezi kwa somo la Kiswahili ili kuwapa hamasa walimu hao.