MKE wa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Maryam Mwinyi, amewaomba wananchi wa Zanzibar kufanya usafi wa mazingira na kupanda bustani katika maeneo yao ili kuweka haiba nzuri ya jiji la Zanzibar .
Aliyasema hayo alipokuwa aizungumza na akina mama wanaopanda miti katika maeneo ya barabara ya mnazi mmoja hospitali hii ikiwa ni miongoni mwa kuelekea siku ya mazingira Duniani.
Alisema wannachi ni vyema kuitunza miti hiyo sambamba na kuhakikisha kuwa wanafanya uwangalizi wa hali ya juu na kutoa elimu kwa wananchi wengine juu ya suala zima la upandaji wa bustani katika maeneo yao kwani kufanya hivo kunaweza kuleta manufaa makubwa kwa vizazi vijavyo .
Aidha aliwapongeza kina mama hao kwa jitihada kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wameanzisha mradi wao wa kupanda bustani na kuuza bustani ambapo pia wameupendesha mji kuonekana wenye haiba bora zaidi.
“Tuendeleeni kutunza mazingira yetu ikiwemo kupanda bustani kwani mji wetu utakuwa mzuri zaidi na hali ya kimazingira utapendeza”
Nae, Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Idrisa Kitwana Mustafa, alisema mkoa wa mjini magharibi umepiga hatua kubwa ya kuweka mazingira safi ya mji na hata kutoa elimu ya usafi wa mazingira kwa kila shehia zilizokuwepo katika mkoa wa mjini magharibi .
Hata hivyo alisema kuwa atahakikisha kila wakati mazingira ya usafi yanakuwa sawa na hata kuzitunza bustani zilizopandwa katika maeneo ya barabara zote .
Hata hivyo, alisema kuwa mabaraza ya manispaa ya mkoa wa mjini magharibi yamekuwa yakifanya usafi wa mazingira kila mara na hata kujitahidi kutoa elimu kwa wananchi wa mkoa wa mjini magharibi .
Sambamba na hayo, Mama Maryam alifanya ukaguzi wa bustani hizo na usafi wa mazingira kuanzia maeneo ya uwanga wa ndege na kumalizikia mnazi mmoja hospitali ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra ya kuelekea kilele cha mazingira Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu “Dunia ni hii moja tu , hifadhi mazingira”
3 comments
Greetings! Very helpful advice in this particular post! It is the little changes that make the most significant changes. Thanks for sharing!
I love looking through a post that will make people think. Also, thanks for allowing me to comment!
Your welcomed