YA MJINI AWAKABIDHI VYETI WALIMU WALIO FANYA VIZURI
Mkuu wa wilaya ya mjini Rashid simai msaraka amesema kuwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ina dhamira ya dhati ya kuhakiksha kuwa ina weka mikakati ya elimu kwa kushiriki anana wadau wa elimu mbalimbali katika wilaya hiyo .
Ame yasema hayo wakati alipokuwa katika zoezi la ugawaji wazawadi kwa walimu waliofanya vizuri kwa walimu wa kidato cha pili kwenda kidato cha tatu 2020 hadi 2021 iliyofanyikakatikaskuliyakidutani .
Amesema kuwa lengo na kutolewa kwa zawadi hizo nikuwapa ari walimu na ufundishaji na kutengamatumizi ya teknolojia katika kufundisha na kujifunza ili kuwe zakupata ufaulu ulio mzuri kwa wanafunzi .
Aidha mkuu huyo amewataka wa mabenk mbalimbali na wafanya biashara kushirikiana kwa pamoja katika kuondosha changamoto za elimu hususani masuala ya madawati na uhaba wa madarasa .
Baadhi ya walimu waliopata zawadi hizo wamewataka walimu wenzao kufundisha kwa uweledi licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi na kuwataka wazazi kushirikiana na walimu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa .
Hata hivyo wamesema kuwa wana matumaini makubwa na wizara ya elimu na mafunzo ya amali katika kuinyanyua sekta ya elimu nchini na kuondosha changamoto zilizokuwemo .