MAJUKUMU YA SEKTA YA USTAWI WA JAMII
Sekta ya Ustawi wa Jamii, wanawake na watoto inatekeleza majukumu mbali mbali miongoni mwa majukumu haya ni:
- Kuratibu na kutekeleza shughuli zote zinazohusiana na ulinzi na hifadhi ya mtoto katika ngazi ya Wilaya
- Kupokea malalamiko na shutuma zinazohusiana na udhalilishaji wa wanawake na watoto, kufanya tathmini mbali mbali na kuandaa taarifa za uchunguzi wa jamii
- Kuratibu utekelezaji wa shughuli za hifadhi za jamii, ikiwemo kutoa msaada kwa wanaoishi katika mazingira magumu, wazee na walengwa wengine
- Kuratibu na kushughulikia masuala yanayohusiana na haki za wanawake na watoto katika ngazi za Wilaya
- Kufuatilia shughuli zinazotekelezwa na taasisi za kiraia , kitaifa na kimataifa katika Wilaya
- Kufanya kazi kwa mashirikiano na maofisa na taasisi zinazofanya kazi za masuala ya ustawi wa jamii
- Kutekeleza majukumu yote tutakayopangiwa na Wilaya na Mkoa