Mkuu wa Wilaya Mjini Mhe. Rashid Msaraka akikagua katika maeneo mbalimbali ya Wilaya Mjini ikiwepo Mpendae, Masumbali na Karakana Chubuni. Lengo la ziara hio ni kuwaweka wachomea grill, wauza mafriji na vitanda waliopo Wilaya Mjini kuwatengezea katika maeneo hayo na ili shughuli zao waje wazifanyie humo. Katika ziara hio pia alitembelea eneo litalojengwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na eneo linalojengwa Hospitali ya Wilaya ya Mjini Unguja. Ziara hio alimalizia Skuli ya Darajani kwa kuzungumza na wafanya biashara wa eneo hilo na kuwaambia eneo la biashara la Skuli ya Darajani tayari ameshamkabidhi Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Mjini kusimamia wafanya biashara hao.