Skuli mpya ya kisasa yafunguliwa ndani ya jimbo la Mpendae, skuli hiyo jina lake ni Salim Turkey Primary School
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameifungua na kusema Serikali yake itaendelea kujenga skuli za kisasa za msingi ili kuondoa msongamano wa wanafunzi madarasani ili Taifa lizalishe wataalamu wazalendo.