UKIMBIZAJI WA MWENGE WA UHURU WILAYA YA MJINI UNGUJA
Mwenge wa uhuru katika wilaya ya mjini Unguja ulikimbizwa na kiongozi wa Mwenge pamoja na viongozi wa wilaya mjini akiwemo Mkuu wa wilaya Ndugu Rashid Simai Msaraka. Mwenge huo ulikimbizwa na kufungua miradi mbalimbali yenye manufaa katika Wilaya hiyo kama vile mradi wa Samaki wa kisasa, mradi wa maji unaotumia sola system, Vijana kukabidhiwa vyeti kwa kuhitimu mafunzo yao, Uzindunzi wa Stone town studio, kwa ajili ya wasanii, uzinduzi wa tovuti wa wilaya ya mjini (yaani website), upandaji wa miti, uzinduzi wa mradi wa chaza na kumalizia Maisara.