Mhe Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka Amepongeza Shirika la Startime kufanya mashindano ya Ligi la daraja la kwaza kwa Vijana wa Mchezo wa Mpira wa Miguu.
Hivyo Ameeleza vijana wengi wameshaanza kujitokeza na kuendelea na Ligi hiyo ya mchezo wa Mpira wa Miguu kwa lengo la kuimarisha Mwili na kukuza vipaji vya Michezo.
Pia ametowa wito kwa Taasisi nyengine kuibuwa michezo mbali mbali ili kuweza kuimarisha Michezo Zanzibar.