Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua Kiwanda cha Basra Textile Zanzibar.
Katika kuadhimisha sherehe za Mapinduzi miaka 58, Mhe. Samia Suluhu Hassan amepongeza ukuaji wa Viwanda kwa maendeleo ya Nchi kwani pamba inayozalishwa Tanzania itauzwa ndani ya Nchi na wakulima watapata faida nzuri, pia nguo zitazoshonwa za kiwango kizuri tutapata kuuza ndani ya Nchi na Nje ya Nchi na Wananchi wa Jimbo la Chumbuni kilipo kiwanda cha Basra Textile wamepata ajira kupitia kuwekwa kiwanda hichi cha ushoni.