Home Habari za kijamii Viongozi wa Serikali ya Mkoa na Wilaya wametakiwa kushrikiana pamoja na Viongozi wa Shehia katika kuipatia ufumbuzi changamoto ya uharibifu wa Mazingira katika eneo la Mpiga Duri.

Viongozi wa Serikali ya Mkoa na Wilaya wametakiwa kushrikiana pamoja na Viongozi wa Shehia katika kuipatia ufumbuzi changamoto ya uharibifu wa Mazingira katika eneo la Mpiga Duri.

by Ally Rutengwe

Viongozi wa Serikali ya Mkoa na Wilaya wametakiwa kushrikiana pamoja na Viongozi wa Shehia katika kuipatia ufumbuzi changamoto ya uharibifu wa Mazingira katika eneo la Mpiga Duri.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alileza hayo kupitia ziara maalum alioifanya ya kukagua eneo la Mpiga duri lililoathiriwa kwa shughuli za ukataji wa Mikoko na uchimbaji wa mchanga.

Alileza kuwa, kuna haja ya kutoa taaluma kwa Wananchi waliolizunguka eneo hilo ili kuwajengea uwelewa juu ya dhana ya uharibifu wa mazingira pamoja na athari zake kwa jamii.

Alisema tatizo la uharibifu wa mazingira katika eneo hilo ni kubwa jambo litakalosababisha athari kwa maji ya bahari kuvamia katika makaazi ya watu kutokana na ukataji ovyo wa misitu aina mikoko sambamba na harakati za uchimbaji wa mchanga.

Mhe. Hemed alifafanua kwamba, Serikali haipendi kuona mivutano baina ya wananchi wake hivyo, amewaagiza viongozi wa Serikali Mkoa, Wilaya na Shehia kuangalia namna bora ya kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo kwa kuwafikishia taaluma wahusika wa vitendo hivyo vya uharibifu wa mazingira.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Pili wa Rais alisema Serikali haitosita kumchukulia hatua mtu yeyote atakaebainika kushiriki katika vitendo vya uharibifu wa mazingira huku akiwaasa wananchi kuachana na vitendo hivyo.

Nae, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dk. Saada Mkuya alisema Jografia ya eneo hilo ni la maficho jambo linapelekea kutumiwa na wahalifu kufanya vitendo viovu ikiwemo shughuli za madawa ya kulevya.

Alisema katika kuhakikisha vitendo vya uharibifu wa mazingira na vitendo vya uhalifu vinatokomezwa katika eneo hakuna budi kupatikana kwa msaada kutoka kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama ili kuidhibiti kadhia hiyo.

Kwa upande wake Sheha wa Shehia ya MuembeMakumbi Halima Azan Makame alimueleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa, eneo la Mpiga duri linakabiliwa na kadhia ya uharibifu wa mazingira kwa muda mrefu sasa  inayosababishwa na wahalifu kutumia zana za jadi kwa kuwashambulia Viongozi wa Shehia wanaofanya Doria katika eneo hilo.

Kufuatia changamoto hiyo Sheha Halima alitoa rai kuwekwa kwa kituo maalum kitakachosaidia katika kuendesha doria katika eneo kwa muda wote.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed ametembelea eneo la Jengo la kihistoria la LIVING STONE liliopo Kinazini.

Mhe. Hemed aliuagiza uongozi wa Wizara ya Fedha kuondosha kibanda kilichokuwa hakitumiki ili kuweka haiba nzuri ya eneo hilo, sambamba na kuweka eneo maalum la kuegesha magari kwa lengo la kuisaidia Serikali kuingiza mapato.

Pia Makamu wa Pili wa Rais aliuagiza Uongozi wa Jumuiya ya kitaifa ya wafanya biashara Zanzibar kuchukua hatua za makusudi kufanya mabadiliko kwa kuwavutia wawekezaji kuja kuekeza Zanzibar.

 

related posts

Leave a Comment