Mkuu wa Wilaya ya Mjini Zanzibar amesema Banda la vyumba viwili lililobomolewa na Manispaa ya Mjini Unguja halikuwa Kanisa kama taarifa zinavyosambazwa katika mitandao ya kijamii Nchini. Banda hilo na mabanda mengine yaliyopakana yamevunjwa ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kuelekea kipindi cha mvua za masika.
Akizungumza na vyombo vya habari Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Rashid Simai Msaraka amesema Mamlaka ya hali ya hewa nchini imeagiza kuchukuliwa kwa tahadhari juu ya Mvua za masika hivyo Wilaya yake imeamua kuvunja Nyumba na Mabanda yote yaliyojengwa bila kufuata sheria. Amesema Banda hilo lililobomolewa na mabanda mengine yote yamejengwa bila kufuata sheria katika maeneo hatarishi jambo ambalo linaweza kusababisha maafa kipindi cha mafuriko.